Mumias: Mtumishi wa Mungu Azomewa kwa Kupendelea Warembo
Kisanga kilitokea katika kanisa moja eneo la Buchinga baada ya majamaa kufokea vikali mtumishi wa Mungu kwa madai alikuwa akiwapendelea akina dada katika mahubiri yake. Mdakuzi alisema kwamba, mara kwa mara, mchungaji alikuwa akiwapendelea sana wanawake wakati akitoa mafunzo yake kanisani jambo ambalo liliwaudhi wanaume.